Kenya news

Wazee wakumbatia mchezo wa mpira wa voliboli – Kenya News Agency

Please log in or register to do it.

Mazoezi yana umuhimu mwingi sana katika mwili wa mwanadamu. Wazee katika mji wa Nyahururu wamekumbatia uchezaji wa voliboli kama njia ya kufanya mazoezi kwa sababu kibao.

Fred Osongo ambaye ni Kocha wa timu ya voliboli mjini Nyahururu anaeleza kuwa yeye na wenzake waliamua kuanzisha mchezo wa voliboli mnamo mwaka juzi. Walianza wakiwa wachezaji wachache lakini kufikia sasa, wamefika wachezaji 40.

Fred anaendelea kusema kuwa sababu kuu iliyowafanya kuanzisha mchezo huu ni haja ya kufanya mazoezi baada ya kazi nyingi za kila siku.

“Sababu kuu iliyotufanya kuanzisha mchezo huu ni kwa sababu ya kufanya mazoezi baada ya kazi kuona kuwa baadhi yetu ni wanabodaboda. Tulipokuwa tukianzisha mchezo huu, tulikuwa wachache sana. Baadhi ya watu walikuwa na mtazamo kuwa mchezo huu ni wa vijana pekee. Wanaume wengi hawakuwa na hamu ya kutuunga mkono katika mchezo huu kwa vile wengi walichukulia kuwa wanaopaswa kucheza ni vijana pekee. Kufikia sasa tumeweza kuvutia wazee wengi na hivi sasa tuko arobaini,” Anaeleza.

Fred anaendelea kusema kuwa mchezo huu umewasaidia sana katika kupunguza uzito wa mwili ili kupigana na magonjwa yanayotokana na uzito wa mwili uliozidi kama kisukari, msisimko wa damu na mengine mengi. Isitoshe, mchezo huu wa voliboli umewasaidia kupata ujuzi mwingi kuhusu sheria za mchezo huu wa wavu.

“Voliboli imetusaidia sana kwa sababu tumeweza kupata ujuzi mwingi kuhusu uchezaji kwa voliboli na pia unasaidia kupunguza uzito kupita kiasi wa mwili ili kupigana na magonjwa yanayotokana na uzito iliokidhiri wa mwili,” anaeleza.

Brian ambaye ni mchezaji wa voliboli anaeleza kuwa umuhimu mkubwa wa mchezo huu wa voliboli ni kuwa huwa haitaji nguvu nyingi wakati wa kucheza hivyo huwa rahisi kuchezwa na wazee. Anaongeza kusema kuwa mchezo huu umesaidia kuleta wazee pamoja hivyo kuendeleza ushirirkiano baina yao.

“Umuhimu wa mchezo huu ni kuwa huwa hauhitaji nguvu nyingi sana kama mchezo wa kandanda wakati wa kucheza hivyo unatufaa sana hasa wazee wa umri wetu. Pia mchezo huu umetusaidia kuja pamoja na kujuana na hili limetusaidia kuunda urafiki kiasi cha kwamba tunaweza kusaidiana iwapo mmoja wetu ana tatizo,” anaeleza.

Mchezo wa voliboli unapaswa kuchukuliwa kwa uzito katika jamii na haswa miongoni mwa watu walio na umri mkubwa. Wanawake pia wanapaswa kuukumbatia mchezo huu ili kukuza vipawa vyao vya kucheza mchezo wa voliboli na pia kwa lengo la kufanya mazoezi.

Na Margaret Wamuyu Kinyua

Related Posts
With 102 Workers Killed, U.N. Agency in Gaza Struggles to Provide Aid

Nearly all of the agency’s funding comes from donations from countries including the United States, Germany and the European Union, Read more

BBC News issues on-air apology for false claim Israel targeting staff and ‘Arab speakers’ at Gaza hospital

BBC News Channel has apologized for an inaccurate report that claimed Israeli forces were targeting "medical teams and Arab speakers" Read more

Kansas elections agency evacuated after receiving suspicious letter

The substance in a suspicious letter sent to the top elections agency in Kansas doesn't appear to have been hazardous, Read more

Shohei Ohtani wins second MVP amid what could be record-breaking free agency

The heavy spring training favorite to win the American League Most Valuable Player Award is taking home hardware again.Shohei Ohtani Read more

Thousands throng Masinde Muliro Stadium for Madaraka Day celebrations
Government commits to solving Nzoia Sugar woes

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *